Kiswahili —

SOS violence conjugale inatoa huduma za hifadhi na rufaa ambazo hutolewa bure, kwa lugha mbili, kwa ufaragha na usiri kwa wahanga wa ukatili wa kimapenzi. Rasilimali hii, ambayo inapatikana saa 24 siku 7 za wiki, inatoa ufikio wa taarifa, usaidizi au huduma za hifadhi katika Quebec yote. Huduma hizi zinapatikana kwa ajili yako na watoto wako.

Huduma za SOS zinapatikana kwa njia ya simu, barua pepe, ujumbe mfupi au soga. Mfanyakazi wa usadizi kutoka SOS daima anapatikana ili kukujibu kwa Kifaransa au Kiingereza, kulingana na lugha ambayo unaipendelea zaidi, lakini baadhi ya wafanyakazi wetu wa usaidizi pia wanazungumza Kihispania, Kiarabu na Kiitaliano. Ukipenda, tutajaribu kutafuta mfanyakazi anayeweza kuwasiliana nawe kwa lugha yako ya asili.

Kuwasiliana na SOS hakukufungi kwenye uamuzi wowote kuhusiana na mwenza wako. Jukumu letu ni kukutaarifu na kukusaidia ili uweze kufanya maamuzi yako mwenyewe katika siku za usoni. Usisite kuwasiliana nasi—tupo kwa ajili yako.

Chat Services

By chat, we can offer you some time to discuss your situation, to be able to explore the resources that could be useful to you in the future. On average, we are available for about 30 minutes per exchange.

How it works?

Begin